Mshambulizi wa zamani wa Liverpool Dean Saunders anaamini Jurgen Klopp atapata majibu ya aliyomnenea Gary Neville alipokuwa Valencia
Gary Neville aliingia kwenye vita ya maneno na Liverpool wiki mbili zilizopita kwa kuukosoa vikali uwezo wa kipa wa timu hiyo Loris Karius.
Mjerumani huyo aliyesajiliwa na Liverpool majira ya joto alijibu mashambulizi kwa kurejea kipindi Neville aliposhindwa kuisaidia Valencia kama meneja, kwa kusema “alikuwa meneja bora kwa kipindi kifupi, na sasa amerejea kuwa mtaalamu tena.”
Jurgen Klopp alimtetea mchezaji wake katika mkutano wa Jumatatu na waandishi wa habari.
“Siwasikilizi,” alisema. “Yeye [Gary] alihaha na kibarua chake kwa kuwahukumu wachezaji [muda mchache ambao hakuwa na mafanikio Valencia] alipokuwa menjea, sasa kwa nini tumruhusu awazungumzie wachezaji kwenye runinga?”
Hata hivyo, Saunders, ambaye alidumu mwaka mmoja Liverpool mapema miaka ya 90, anaamini Klopp alichemka kukumbushia mambo ya Neville alipokuwa Valencia kwani hata yeye yupo hatiani kufukuzwa Liverpool siku moja watakapotaka kubadili meneja.
“Nadhani Gary Neville alikuwa sahihi kwa kile alichosema, kwani hajaongea kwa upendeleo, yeye ni mchezaji wa zamani wa Manchester United dhidi ya Liverpool,” Saunders alikiambia talkSport.
“Na Jurgen Klopp alikuwa sahihi kuendelea na kipa wake, lakini nadhani alimshambulia zaidi Gary Neville kuhusu kibarua chake cha Valencia.
“Siku moja atatupiwa virago na Liverpool na tutamuona kwenye TV na mtu mmoja atasema maneno hayo hayo dhidi yake: ‘unawezaje kusema chochote utakapofukuzwa kazi na Liverpool? Umechemka’.
“Kama meneja ipo siku utatupiwa virago.”
Klopp amekuwa na timu ya Liverpool kwa miezi 14 sasa tangu alipoichukua nafasi ya Rodgers Oktoba mwaka jana. Mjerumani huyo ameleta mabadiliko makubwa kwa klabu hiyo akiifikisha kwenye fainali za michuano miwili msimu uliopita.
Liverpool pia wameimarika sana kulingana na msimu uliopita kwani wanaweza kupanda nafasi ya pili iwapo watashinda dhidi ya Middlesbrough jioni hii.

0 Maoni:
Post a Comment