Ommy Dimpoz amefunguka kuzungumzia ushindani uliopo kwenye muziki wa sasa na kipindi ameingia kwenye tasnia hiyo.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo “Kajiandae” akiwa na Alikiba amesema kuwa presha za mashabiki ndio zinasababisha nyimbo za wasanii kupotea mapema na kuwafanya waachie nyimbo nyingi kwa muda mfupi tofauti na zamani ilivyokuwa.
“Unajua ushindani wa sasa hivi na wazamani umebadilika. Zamani ulikuwa unaweza kutoa wimbo kwa muda mrefu ukakaa lakini sasa hivi imekuwa watu wiki nyimbo, wiki nyimbo japo mimi siupendi sana huo utaratibu kiukweli,” Ommy amekiambia kipindi cha The Playlist cha Tmies FM.
“Naona si utaratibu mzuri kwa sababu hauzipi nyimbo zako nafasi, unainvest matokeo yake nyimbo zinakufa mapema. Tusifanye nyimbo kwa presha yaani sometimes mashabiki pia wanatupa presha sana, inabidi waelewe kwamba kuna kuinvest hela nyingi, shabiki anachotaka yeye raha umridhishe lakini pia shabiki anatakiwa aelewe video zinacost hela nyingi,” ameongeza.
Dimpoz ameongeza kuwa walau msanii anatakiwa atoe nyimbo kila baada ya miezi mitatu ili kuzipa nafasi nyimbo zake nyingine zilizopita.
0 Maoni:
Post a Comment