Serikali kuanzisha Passport za kieletroniki na uhamiaji wa mtandao

tanzania-passport
Serikali imepanga kuanzisha mfumo wa uhamiaji wa mtandao pamoja na hati za kusafiria ‘Passport’ za kieletroniki.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba alipotembelea makao makuu ya Idara ya Uhamiaji, Nyumba za Makamishna wa Uhamiaji na Kiwanda cha Uhamiaji cha Uchapaji wa Nyaraka kilichopo Mtoni-Kijichi jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuona utendaji kazi wa idara hiyo.
Katika ziara yake hiyo, Nchemba amesema ili kuboresha huduma za uhamiaji na kuondoa usumbufu kwa wananchi, serikali kupitia kikao kilichopita cha Bunge imeweka maazimio ya kuanzisha uhamiaji wa mtandao pamoja na hati za kusafiria ‘Passport’ za kieletroniki.
Hata hivyo, baada ya kusikiliza malalamiko ya wananchi kuhusu ucheleweshwaji wa utolewaji wa hati za kusafiria, Waziri Nchemba ametoa maagizo kwa idara hiyo ikiwa ni pamoja na kuitaka kuanzisha mfumo wa malipo wa kieletroniki ili kupunguza ucheleweshwaji wa malipo pamoja na kuzuia mianya ya upotevu wa fedha.
Pia Nchemba ameahidi kuwasiliana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kufanya marekebisho ya baadhi ya vifungu vya sheria visivyotambua wazawa waliozaliwa nchini na wageni kama raia halali licha ya wageni hao kuishi miaka mingi.
Pia ameitaka idara ya uhamiaji kuboresha masilahi ya watumishi wake ikiwa ni pamoja na kuwapa fedha za ruzuku ya makazi, kulipa madeni na kupandisha misharaha ya watumishi waliopanda vyeo.
“Pamoja na maelekezo hayo, wale wanaoshughulikia taarifa za watumishi wawajibike, kutekeleza mahitaji ya watumishi wajue kwamba hilo suala si hisani bali lipo kwa mujibu wa sheria,” amesema.
Kuhusu nyumba za makamishna wa uhamiaji, mradi wake ulianza katika mwaka wa fedha wa 2012/2013 kwa awamu na kwamba uko katika hatua za mwisho.

Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment