ARGENTINA YALIPA KISASI KWA COLOMBIA YAIBAMIZA 3-0 KUFUZU KOMBE LA DUNIA.

argentine-players-celebrate-after-beatin
Baada ya kufungwa magoli matatu na Brazil hatimaye Leo timu ya Argentina wameibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Colombia mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Estadio De Bicentenario wa kuwania nafasi ya kufuzu kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Argentina walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa nahodha na mchezaji wa kutengemea wa klabu ya Barcelona Lionel Messi dakika ya 10 akifunga goli safi akitumia udhaifu wa mabeki wa Colombia na kuwanyanyua mashabiki wa Argentina waliofurika katika uwanja huo.
Lucas Pratto aliifungia tena Argentina magoli mawili ya haraka haraka katika dakika za 23 na 28 na kuwafanya Colombia wapotee kwa kuchanganikiwa na hayo magoli matatu hadi timu zinaenda mapumziko wenyeji walikuwa mbele kwa magoli matatu kwa bila.
Kipindi cha pili kilikuwa kigumu kwa kila timu kwani zilishindwa kufungana na Colombia wakishindwa hata kupata goli la kufutia machozi hadi mwamuzi toka nchini Eduardor ,Zambrano anamaliza mpira Argentina wameibuka na ushindi wa magoli 3-0 na kuwapandisha juu ya msimamo.
Sasa Argentina imepanda hadi nafasi ya tano wakiwa na pointi 19 huku Colombia nao wakishuka chini nafasi ya sita wakiwa na pointi 18 na matokeo mengine,Eduador 3-0 Venezuela,Chile 3-1 Uruaguay,Peru 0-2 Brazil.
VIKOSI:
Argentina: Romero; Mercado, Otamendi, Funes Mori, Mas; Mascherano, Biglia; Di Maria (Acuna 85′), Banega (Perez 63′), Messi; Pratto (Higuain 79′)
Subs: Roncaglia, Rulli, Guzman, Pizarro, Demichelis, Correa, Zabaleta, Belluschi, Aguero.
Goals: Messi, Pratto.
Booked: Funes Mori, Mercado, Banega, Pratto  
Colombia: Ospina; Arias, Sanchez, Murillo, Balanta; Sanchez, Cuadrado, Torres (Copete 67′), Barrios (Torres 46′), Rodriguez; Falcao (Bacca 76′) 
Subs: Cardona, Perez, Gonzalez, Muriel, Vargas, Medina, Borja, Diaz, Aguillar.
Booked: Alvarez, Arias, Rodriguez, Cuadrado 
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment