Mahakama ya juu nchini Misri imetengua adhabu ya hukumu ya kifo dhidi ya Rais wa zamani wa nchi hiyo aliyeondolewa madarakani Mohammed Morsi.
Morsi alihukumiwa adhabu ya kifo kwa ushiriki wake wa kuvunja gereza na wafungwa kutoroka kulikofanywa mwaka 2011 wakati wa vuguvugu la mabadiliko lililoikumba nchi hiyo.
Alichaguliwa kuwa Rais wa nchi hiyo mwaka 2012, lakini aliondolewa madarakani katika mapinduzi ya kijeshi dhidi ya utawala wake kufuatia maandamano makubwa yaliyofanyika nchini humo kuupinga utawala wake.
Kwa nyakati tofauti Morsi alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya ugaidi na bado anakabiliwa na mashitaka mengine.
0 Maoni:
Post a Comment