Guardiola huwakataza wachezaji kufanya mapenzi baada ya saa 6 usiku – Nasri

samir-nasri-premier-league-manchester-city_3037007

Mchezaji wa Ufaransa katika safu ya kati Samir Nasri amefichua kwamba mojawapo ya ufanisi mkubwa wa mkufunzi Manchester City Pep Guradiola ni kuwaagiza wachezaji wake kutofanya mapenzi baada ya saa sita usiku.
Katika mahojiano na runinga ya Ufaransa, Nasri amesema kuwa Guardiola aliweka sheria hiyo hata iwapo kungekuwa hakuna mechi siku iliofuatia ili wachezaji wapate usingizi mwanana.
Hata Lionel Messi anayetambulika kuwa mchezaji bora duniani hakuwachwa nje wakati wa uongozi wa Guradiola katika timu ya Barcelona.
Nasri amesema kuwa hatua hiyo ilimwezesha Messi kutopata majeraha ya misuli
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment