WANANCHI NA VIONGOZI WA KATA KATIKA MKUTANO WA HADHARA
MWENYEKITI KIBWABWA B KATIKATI HAMIS MHEHE KUSHOTO KWAKE DIWANI WA KATA YA KITWIRU MHE. BARAKA KIMATA NA KULIA NI AFISA MTENDAJI WA KATA SALUM UPETE
BAADHI YA AKINA MAMA WALIOFIKA KATIKA MKUTANO HUO
MHE. BARAKA KIMATA DIWANI AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WAKE
Na Dajari Mgidange, Iringa
Wananchi wa Kata ya Kitwiru
Manispaa ya Iringa wanamsubiri kwa hamu ujio wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dr. John Pombe Magufuli katika sherehe za wafanyakazi Mei Mosi.
Katika sherehe hizo ambazo
hufanyika kila mwaka Tarehe Moja mwezi wa Tano ambapo Kitaifa zinatarajiwa
kufanyika Mkoani Iringa na kwa mara ya kwanza tangu kuchaguliwa kwa Rais
Magufuli atakuja Mkoani hapa kama mgeni Rasmi wa Maadhimisho hayo.
Wakizungumza katika Mkutano
wa hadhara uliofanyika katika kata hiyo jana Jumamosi ya Tarehe 14/04/2018 na
kuhudhuriwa na Diwani wa Kata hiyo Mhe. Baraka Jeremiah Kimata, wananchi hao
wameonesha kufurahishwa na kusikia ujio wa Mheshimiwa Rais.
“Mimi nimefurahishwa sana na
nimepokea kwa shangwe kubwa kuja kwa Mhe. Rais kwani kutafungua fursa kwa sisi
akina mama kwa kuhudhuria na kufanya Biashara zetu mbalimbali”. Alisema Bi
Fatuma Kasirani Mwananchi wa Kta hiyo.
Mwenyekiti wa Mtaa wa
Kibwabwa B Hamis Mhehe maarufu kwa jina la “Balaa” amewasihi wananchi wake kujitokeza
kwa wingi katika siku hiyo ya wafanyakazi ikiwa ni mara yake ya kwanza kufika
Mkoani Hapa tangu Achaguliwe kuwa Rais Mwaka 2015.
Kwa upande wake Diwani wa
Kata hiyo Mhe. Baraka Kimata amesema
kuwa Rais Magufuli na sera yake ya “Hapa Kazi tu” imeleta chachu ya maendeleo
na usawa katika jamii yetu kwani amepunguza “Gap” lililokuwepo kwa matajiri na
masikini waliokuwa wakitumia pesa ovyo.
“Mwanzo tulizoea kula vitu vya
dili lakini sasa kila mtu anakula kile alichokitafuta mwenyewe na zamani
tulilalamika kuwa awamu iliyopita Rais alikuwa akisafiri sana lakini awamu hii
Rais ameamua kutulia nyumbani na ndio maana watu haweleti mzaha”. Alisema
Kimata.
Aidha Kimata amewataka
wananchi kujitokeza kwa wingi katika sherehe hizo za Mei Mosi kwa wale
waliomchagua Rais na hata ambao hawakumchagua na kuwasisitizia kuwa hata yeye pia
atakwenda kumuona katika maadhimisho hayo.
Katika Hatua nyingine
amewaomba wananchi kutoa ushirikiano katika maendeleo ya kata hiyo hasa katika
swala la ulinzi na usalama wao kwa kuwafichua Wahalifu wanaofanya uhalifu
katika majumba ya watu na maduka.
Naye Afisa Mtendaji wa Mtaa
wa Kibwabwa “B” Bw. Salum Upete katika swalala ulinzi na usalama amewataka
wananchi wa kata hiyo kutoa ushirikiano wa zoezi la uandikishwaji wa wakazi wa
maeneo hayo ikiwa ni katika swala la utambuzi ili linapotokea swala la Uharifu
waweze kutambuana.
Siku chache zilizopita
katika Kata hiyo Kumekuwa na matukio ya uhalifu ya uvamizi wa maduka na nyumba
za watu na kuibwa kwa vitu mbalimbali vya maduka na nyumba za wananchi wa
Kitwiru.
Rais Magufuli anatarajiwa
kuwa Mgeni rasmi katika Sherehe za Mei Mosi zitakazofanyika Kitaifa Mkoani Hapa
tarehe moja Mei na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali watakaofika Mkoani hapa
katika sherehe hizo.
0 Maoni:
Post a Comment