Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa hakuna uwezekano wowote kwamba mshambuliaji wa Misri Mo Salah atauzwa mwisho wa msimu huu
Salah ameifungia Liverpool mabao 39 msimu huu tangu ajiunge na timu hiyo huku akiwa kinara wa mabao wa ligi ya Uingereza inayoelekea ukingoni akifuatiwa na kiungo wa Tottenham Hotspurs Harry Kane.
Mchezaji huyo amekuwa akiwaniwa na vilabu vikubwa Duniani kama Real Madrid ambao wameonesha nia ya kutaka kumsajili
0 Maoni:
Post a Comment