Rais wa TUCTA Tumaini Nymhokya katikati akizungumza na waandishi wa Habari
Na Dajari Mgidange,
Rais wa Jmhuri ya muungano
wa Tanzania Dr John Pombe Joseph Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
maadhimisho ya siku ya wafanya kazi Mkoani Iringa.
Katika mkutano wake na
waandishi wa habari Mkoani hapa Rais wa TUCTA bwana Tumaini Nyamhokya amesema
kuwa kuelekea siku hiyo ya wafanyakazi Mei Mosi Iringa kutaambatana na matukio
mbalimbali ikiwemo semina na makongamano yatakayofanyika katika wilaya zote za
Iringa.
“Kutakuwa na makongamano
mawili ya Kimkoa na moja la Kitaifa , Kongamano la kwanza litafanyika tar
23.04.2018 katika wilaya ya Mufindi na Kongamano la pili litafanyika tar
25.04.2018 Wilayani Kilolo na tar 27 mwezi huu kutafanyika Kongamano kubwa la
Kitaifa litakalohusu Tanzania na Uchumi wa Viwanda katika ukumbi wa kichangani
Manispaa ya Iringa”. Alisema Nyamhokya.
Nyamhokya amesema kuwa
kutakuwa na michezo ya Mei Mosi ya fani mbalimbali itakayoanza tarehe 16 mwezi
huu wanne mpaka tarehe 30 mwezi huu ambayo itakuwa ikifanyika katika viwanja vya
Samora na Mkwawa.
Kila mwaka sherehe hizi
hufanyika na huambatana na ujumbe na mwaka huu katika maadhimisho hiyo ujumbe
unasema "KUUNGANISHWA KWA MIFUKO YA
HIFADHI YA JAMII NCHINI KULENGE KUBORESHA MAFAO YA WAFANYAKAZI".
Hii itakuwa mara ya kwanza
kwa Rais Dr. John Pombe Magufuli kutua Iringa tangu kuchaguliwa kwake kuwa Rais
mwaka 2015
0 Maoni:
Post a Comment