Wasanii wa filamu nchini Tanzania wakiwakilishwa na Steve Nyerere pamoja na Aunt Ezekiel Jumatano hii wamemtembela muigizaji mkongwe nchini, King Majuto, ambaye amelazwa katika Hospitali ya Tumaini iliyopo Upanga Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya kumjulia hali hospitalini hapo Mwenyekiti wa Wasanii, Steven Mengele ‘Steve Nyerere’, amesema kutakuwa hakuna haja ya wasanii hao kutoa michango mikubwa mara tu, mzee Majuto atakapopoteza maisha, kwahiyo wamejipanga na kumtafutia tiketi mbili ili aweze kwenda India kupata matibabu.
0 Maoni:
Post a Comment