MKWASA AELEZA MBINU WATAKAZOTUMIA KUTWAA MAMILIONI YA CAF ETHIOPIA

Charles Boniface Mkwasa, Kocha msaidizi wa kikosi cha Yanga
Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa, ameelezea namna maandalizi ya kambi kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Wolaitta Dicha FC.

Mkwasa amesema hali ya wachezaji inaendelea vizuri hivi sasa na wamejipanga kupata matokeo katika mechi hiyo itakayopigwa Aprili 18 2018.

Katibu huyo ameeleza watakuwa na mbinu ya kulinda matokeo ili wasiweze kurudishiwa mabao mawili ambayo walishinda katika mechi ya mkondo wa kwanza.

Yanga itahitaji sare pekee ama ushindi wowote ili kuweza kusonga mbele kuingia hatua ya makundi na kutwaa kitita cha milioni 600 endapo itafuzu.

Tayati kikosi hicho kilianza mazoezi jana na leo kitaendelea kuelea mtanange huo.
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment