Mwenyekiti
wa Mtandao wa Wanafunzi nchini ABDUL NONDO ambaye pia ni Mwanafunzi wa Chuo
Kikuu Dar es Salaam UDSM aliye ripotiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha
amepatikana akiwa hai eneo la Mafinga mkoani Iringa.
Akithibitisha
kupatikana kwa Mwanafunzi huyo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Iringa RPC
JUMA BWILE amesema jana majira ya saa 1 ABDUL alifika kituo cha Polisi Mafinga
Wilayani Mufindi na kueleza kuwa alitekwa na watu wasiofahamika.
Amesema Abdul Nondo ni kijana mwenye umri wa miaka 24 na anasoma shahada yake ya kwanza kitivo cha Siasa na Utawala katika Chuo kikuu Dar Es Salaam ambako hivi karibuni alipotea katika mazingira ya kutatanisha jijini humo.
"Kijana huyu amepatikana akiwa salama akiwa hana jeraha lolote lile kama ambavyo mnamuona na mpaka uchunguzi utakapokamilika ataruhusiwa kuzungumza ila kwa sasa yupo kwenye uchunguzi" Alisema Kamanda Bwile.
Aidha
Kamanda BWILE amesema wanaendelea kufanya uchunguzi wa tukio hilo na endapo
kama ametoa taarifa za uongo watamshughulikia kama wahalifu wengine.
Tazama tukio zima Abdul Nondo akifikishwa Makao makuu ya Polisi Leo hapa Mkoani Iringa
0 Maoni:
Post a Comment