KuliaMwenyekiti Wa UWT Kijiji cha Itulahumba akiwa mstali Wa mbele katika maandamano hayo.
Ikiwa leo ni siku ya
maadhimisho wanawake Duniani ambayo kila mwaka hufanyika tarehe 08 mwezi machi ambapo
kwa mwaka huu maadhimisho hayo kwa Mkoa wa Njombe yamebebwa na kauli mbiu
isemayo KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA TUIMARISHE USAWA WA KIJINSIA NA UWEZESHAJI
WA WANAWAKE VIJIJINI.
Kwa Mkoa wa Njombe Katika
Wilaya ya Wanging’ombe kata ya Italumba maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani
yameadhimishwa kwa maandamano yaliyobebwa na ujumbe wa mabango mbalimbali.
Akizungumza Mgeni rasmi wakati
wa Maadhimisho hayo, mwakilishi wa Mkurugenzi mtendaji wa Wilaya ya
Wanging’ombe Ndugu Mansoor Said
Ngenzi amewataka wanawake wa kata hiyo kusimama imara na kuwa mstari Wa mbele
katika kuelekea Uchumi Wa Viwanda kwani haki ni sawa kwa wote pasipo na ubaguzi
wowote.
Aidha Ngenzi amewataka wanawake kuzijua haki zao za msingi katika
shughuli za maendeleo zitakazowaondolea migogoro isiyo na misingi katika jamii
wanazoishi.
Kadhalika, Mkurugenzi huyo amewataka wananchi hao wa kata hiyo kutoa
taarifa ya vitendo mbalimbali vya kikatili vinavyoendelea majumbani mwao
ambavyo mara nyingi wamekuwa wakivifumbia macho kwa vitisho na waume zao.
Katika hatua nyingine Ngenzi Amewataka wazazi wote wa kata hiyo
kuwapeleka watoto wote shuleni ambao wamefikia umri wa kwenda shule kwani
Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dr John Pombe Magufuli imedhamiria kwa
dhati wanafunzi wote kusoma bure.
“Hakikisheni watoto wote mnawapeleka mashuleni hata wale wenye watoto
watoro warudishwe haraka kuendelea na masomo”. Alisema Ngenzi.
Baada ya kuyasema hayo, Mkurugenzi alitoa zawadi kwa watoto yatima ikiwa ni Sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.
0 Maoni:
Post a Comment