Michuano ya Klabu bingwa Ulaya imeendelea tena jana Jumatano kwa michezo miwili Manchester city wakiwa nyumbani Etihad wamebanwa mbavu na Fc Basel baada ya kukubali kuchapwa bao 2-1.
Man city ndio walikuwa wa kwanza kuliona lango la Fc Basel kwa bao la dakikaya 8 kipindi cha kwanza likifungwa na Gabriel Jesus huku Fc Basel wakisawazisha bao hilo dakika ya 17 likifungwa na Mohamed Eliounoussi na Michael Lang akiandikia bao la pili Basel dakika ya 71 kipindi cha pili.
Kwa matokeo hayo Manchester city wanasonga mbele katika hatua ya robo fainali kwa idadi ya magoli 5-2, Mchezo mwingine Tottenham hotspurs wakiwa dimba kongwe la Wimbley wamechapwa na Juventus bao 2-1, Bao la Tottenham limefungwa na Son Heung-min huku Juventus wakisawazisha bao kupitia kwa Gonzalo Higuan bao la pili lililofungwa na Paulo Dybala dakika ya 67 kipindi cha pili.
Matokeo hayo yanaipeleka hatua ya robo fainali Juventus kwa ushindi wa mabao 4-3, Michezo mingine itaendelea tena wiki ijayo kwa michezo miwili, Manchester United itacheza na Sevilla , As Roma watawakaribisha Shakhtar Donetsk, Barcelona ni wenyeji wa Chelsea.
0 Maoni:
Post a Comment