Wananchi
wa jimbo la Mtama mkoani Lindi wamemhoji mbunge wao, Nape Nnauye kuhusu
ndege aina ya Bombardier, wakitaka kujua inawasaidiaje.
Ndege
mbili aina ya Bombardier Dash 8 Q400 zilinunuliwa na Serikali kwa ajili
ya kulifufua shirika la usafiri wa anga la Air Tanzania (ATCL), ambalo
lilikuwa limezorota na kutishia uhai wake.
Ndege hizo zilizinduliwa na Rais John Magufuli Septemba 28, 2016 jijini Dar es Salaam.
Lakini
wananchi wa Mtama bado hawajaona umuhimu wake na walimuhoji Nape,
ambaye alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Jana Nape aliandika katika akaunti yake ya Twitter kuhusu utashi huo wa wananchi wake kuhusu Bombardier.
“Watu hawa wanapambana na hali zao! Waliniuliza bombardier ndiyo nini” na sie wa vijijini tutafaidikaje au ni kwenu mjini tu!?” ameandika Nape katika akaunti hiyo.
Alipoulizwa
, Nape aliyewahi kuwa katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, alithibitisha
kutuma ujumbe huo, akisema ni swali aliloulizwa na wanakijiji.
“Mimi
sijui kwa nini mnauliza sana hicho kitu.Mimi nilikuwa jimboni kwangu
nazungumza na wananchi kuhusu korosho, mwanakijiji mmoja akauliza kwamba
hiyo Bombardier ina faida gani? Na mimi nimeripoti maneno yake. Si
maneno yangu.
“Suala
si mimi kuwa na cheo, mimi ni mbunge wa wananchi. Hilo swali hata wewe
ukiliuliza hapo mtaani utapata majibu matano tofauti.
“Nilikuwa
nazungumza na wanavijiji kuhusu fedha zinazotolewa na Serikali kuhusu
korosho, mbaazi na mazao mengine, ndipo nikaulizwa na mimi nimeripoti
kwa rafiki zangu nilivyoulizwa.”
Lindi
na Mtwara ni kati ya mikoa iliyokuwa inafikika kwa shida kabla ya
Serikali kujenga barabara zilizorahisisha usafiri. Pamoja na usafiri wa
barabara, Air Tanzania imeanzisha usafiri wa anga kwa ajili ya kuhudumia
wasafiri wengine kwenda na kutoka mikoa hiyo ambayo hivi sasa
inachangamshwa na uwekezaji katika gesi na viwanda vya saruji.
0 Maoni:
Post a Comment