Klabu ya Mbeya City na kocha Kinah Phiri wamejikuta wakitofautiana baada ya taarifa kusambaa kwamba kocha huyo kavunja mkataba wa kuitumikia klabu hiyo.
Akizungumza na dmgidange.blogspot.com, kocha huyo amesema walikaa kikao na uongozi na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala na kukubaliana baadhi ya vitu kabla ya kuvunja mkataba.
“Taarifa zimetoka kuwa mimi nimevunja mkataba, kilichopo ni kuwa sijapokea pesa bali ni makubaliano bado hawajavunja mkataba na mimi, nawadai miezi 18 lakini wakawa hawana pesa ikabidi nipunguze mpaka miezi mitatu lakini bado wameniambia mpaka wapokee pesa za mechi (gate collection), ndio wanipatie,” Phiri.
Msemaji wa klabu hiyo Shah Mjanja amefafanua kuwa timu hiyo imefikia hatua ya makubaliano ya pande mbili na kumalizana kila kitu na kocha huyo.
“Kikao ambacho walikaa bodi na kocha tayari walishakubaliana kila kitu na kuafikiana kuvunja mkataba, kinachofanyika hivi sasa ni kulipa pesa ambazo anatakiwa apewe,” Mjanja.
Inadaiwa kuwa kocha huyo anadai malimbikizo ya mshahara na fidia katika timu hiyo kiasi kinachotajwa kukaribia milioni 40.
0 Maoni:
Post a Comment