Mshambuliaji Harry kane alifunga
mabao mawili huku Tottenham ikiishinda Borussia Dortmund na hivyobasi
kupiga jeki matumaini yao ya kombe la vilabu bingwa Ulaya katika uwanja
wa Wembley.
Bao lake la kwanza liliwawacha Dortmund bila jibu baada ya kutamba na mpira kutoka upande wa kushoto wa uwanja kabla ya kucheka na wavu dakika 15 katika kipindi cha kwanza baada ya bao la dakika ya 11 la Son Hueng-min kusawazishwa na mshambuliaji wa Dortmund Andriy Yarmolenko.
Bao la pili la Kane ulikuwa mkwaju wa kimo cha nyoka katika dakika ya sitini na hivyobasi kuipatia timu yake motisha ya kukabiliana na tishio la wapinzani wao waliotawala mechi hiyo.
Hatahivyo Tottenham walimaliza mechi hiyo wakiwa wachezaji 10 baada ya beki Jan Vertonghen kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumshika mchezaji wa ziada wa Dortmund Mario Gotze.
0 Maoni:
Post a Comment