Wakati
Mtuhumiwa wa matukio ya utekaji watoto, Samsom Petro (18), ambaye jana
alifikishwa Arusha kwa ajili ya kuonyesha sehemu alipowaficha watoto,
amebainika kuwa anaishi na kaka yake ambaye ni askari wa Kikosi cha
Kutuliza Ghasia (FFU) cha mjini hapa.
Inadaiwa
kuwa askari huyo pia anashikiliwa na polisi kwa mahojiano tangu Agosti
27 wakati kikosi maalum cha polisi kilipozingira nyumba aliyopanga.
Petro,
ambaye alikamatwa juzi akiwa Katoro mkoani Geita, anatuhumiwa kuwateka
watoto wawili, Moureen David(6) na Ikram Salim(3) na hadi jana jioni
alikuwa ameandamana na polisi katika eneo la Njiro ambako alidai
aliwatelekeza watoto hao.
Lina Kajuna ambaye ni mmiliki wa nyumba ya aliyekuwa amepanga askari huyo wa FFU, alisema ana miaka miwili tangu ampangishe.
Kajuna
alisema mtuhumiwa wa utekaji, Samson Petro alifika Arusha mwezi Juni na
amekuwa akiishi na kaka huyo na tangu amefika amekuwa akimuona kuwa na
tabia ambazo sio nzuri, kama wizi wa kuku.
“Alipofika
muda mfupi tulianza kuona matukio ya wizi nikaibiwa kuku na pesa mimi
nikamlalamikia kaka yake lakini akasema tuendelee kumchunga,”alisema
Alisema
baada ya hali ya wizi kuendelea, alikwenda kulalamika kwa balozi wa
eneo wanaloishi ambalo ni Mtaa wa Olkeria, Daniel Kichau kutaka
wamchunguze.
Hata
hivyo, alisema wakati akichunguza, ndio matukio ya utekaji yakaanza na
tangu Agosti 25 alitoweka nyumbani hadi jana walipopata taarifa kuwa
amekamatwa.
Akizungumzia
tukio hilo, mwenyekiti wa Mtaa wa Olkerian, Daudi Safari alisema jana
kuwa kikosi chao cha wananchi walifika kwenye nyumba hiyo na kubaini
alikuwa anaishi na askari huyo wa FFU .
“Tumemuhoji
mama mwenye nyumba ametupa ushirikiano mkubwa na ni kweli Samson
alikuwa anaishi kwenye nyumba yake na kaka yake ambaye alikamatwa tangu
Agosti 27,” alisema.
Katika
msako wa jana, polisi walikwenda peke yao na mtuhumiwa na kuwaacha
wazazi wa watoto hao wakiwasubiri kituo kikuu cha polisi. Baadhi ya
askari walisema wanaendelea na msako wa watoto hao
0 Maoni:
Post a Comment