Matukio
ya utekaji watoto mjini Arusha yameanza kupata mwelekeo wa ufumbuzi
baada ya kijana wa miaka 18 kukiri kuwateka watoto wanne alipokamatwa
katika mji wa Katoro wilayani Geita alikofanya tukio jingine la utekaji.
Akizungumza
mbele ya waandishi wa habari akiwa chini ya ulinzi wa polisi jana,
kijana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Samson Petro alisema watoto
wawili aliwarudisha kwa wazazi wao baada ya kupewa Sh300,000.
Alisema wengine wawili aliwatelekeza mtaani baada ya wazazi wao kutotoa kiasi cha fedha walichotakiwa kumpa.
Samson
alisema alianza ‘shughuli’ hiyo ya utekaji watoto kutokana na mahitaji
ya fedha na kwamba, aliacha shule akiwa kidato cha tatu katika Shule ya
Sekondari Lutozo iliyopo Katoro.
“Naishi
na wazazi wangu, lakini nao ni masikini, nilifanya hivi ili nipate
fedha na nilikuwa nikimchukua mtoto naandika ujumbe kwenye karatasi,
naandika na namba ya simu napeleka karibu na familia ili wanitafute,”
alisema Samson.
Awali,
kamanda wa polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo alisema
walimkamata kijana huyo katika nyumba ya kulala wageni ya Shitungulu
iliyopo mjini Katoro juzi saa mbili usiku.
Mwabulambo
alisema polisi mkoani Geita kwa kushirikiana na wenzao wa Arusha
walifanya uchunguzi na kubaini mtuhumiwa alikuwa Katoro.
Alisema
walipata taarifa za kutekwa Justin Ombeni (2) Septemba Mosi nyumbani
kwao katika eneo la Shilabela ambako mtuhumiwa alikwenda na kuwakuta
watoto wanne wakicheza nyuma ya nyumba.
Alisema
aliwagawia pipi na kuondoka na Justin. Kamanda huyo alisema polisi
ilipata taarifa kuwa kijana huyo yupo chumba namba 103 katika nyumba
hiyo ya wageni ambako waliweka ulinzi kuizunguka.
Alisema walipoingia katika chumba hicho walimkuta akiwa na
mtoto huyo. Mwabulambo alisema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.
Ombeni
Mshana ambaye ni baba wa Justin alisema mtekaji huyo alimpatia ujumbe
mtoto wa jirani uliomtaka kutuma Sh4 milioni na walipokuwa wakiwasiliana
na mtuhumiwa alishusha kiwango hadi Sh1 milioni.
Alisema
polisi walimtahadharisha kwamba asitume fedha hizo.Kamanda Mwabulambo
alisema tukio la kutekwa Justin ni la pili katika kipindi cha miezi
minne baada ya mwingine kutekwa.
Kesi kuhusu tukio hilo la kwanza inaendelea mahakamani baada ya mtoto kupatikana.
Katika
hatua nyingine, kikosi kilichoundwa na wananchi mkoani Arusha
kikiongozwa na mwenyekiti wa Mtaa wa Olkerian, Kata ya Olasiti, Daudi
Safari na familia za watoto wawili waliotekwa kimewakamata watuhumiwa
wawili na kuwafikisha polisi.
Watoto
hao ambao bado hawajapatikana ni Moureen David (6) anayesoma darasa la
kwanza shule ya msingi Lucky Vincent na Ikram Salim (3).
Wakizungumza
jana nje ya kituo kikuu cha polisi Arusha baada ya kuwafikisha kituoni
watuhumiwa hao, Safari na wazazi wa watoto hao, David Njau na Salim
Kassim walisema kwa nyakati tofauti wameanzisha msako baada ya
kuona siku zinakwenda bila watoto kupatikana.
Moureen
alitekwa Agosti 21 saa 11 jioni akiwa anacheza nyumbani kwao eneo la
Olasiti, wakati Ikram alitekwa Agosti 26 saa 12 jioni akiwa anacheza na
watoto wenzake nyumbani kwao, Burka - Olasiti.
Safari alisema wamemkamata mtu mmoja (jina linahifadhiwa)
ambaye simu yake ilitumiwa na watekaji kuomba fedha kwa mzazi wa Ikram Salim.
Alisema
pia wamemkamata wakala wa fedha wa kampuni moja ya simu (jina
tunaihifadhi) aliyetoa Sh300,000 kwa watekaji baada ya fedha kutumwa na
mzazi wa Ikram.
Imeelezwa
kuwa wakala huyo amekamatwa kwa kuwa fedha hizo zilitolewa pasipo
kuorodheshwa popote na mpokeaji hakuonyesha kitambulisho chochote.
Akizungumzia operesheni hiyo, Njau alisema hawatapumzika mpaka watoto wao wapatikane.
Alisema
ufuatiliaji walioufanya kupitia minara ya kampuni za simu unaonyesha
wahusika walikuwa eneo la Kwa Mrombo jijini Arusha walipopiga kuomba
Sh4.5 milioni ili wamwachie Doreen na kiasi kingine kama hicho kwa ajili
ya Ikram.
Watekaji
hao kupitia ujumbe waliotuma nyumbani kwa Njau walidai kama wasipopewa
fedha wangempoteza mtoto huyo japokuwa hawana nia hiyo.
Kassim
Salim ambaye ni babu wa Ikram alisema, “tunaendelea kuomba msaada zaidi
kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na vyombo vya dola
watusaidie tuwapate watoto wetu.”
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema juzi kuwa watu watatu
wanashikiliwa wakihusishwa na tukio hilo akiwapo dereva wa bodaboda
mkazi wa Olasiti aliyetumwa kuwarejesha watoto wawili waliokuwa
wametekwa.
Matukio
ya utekaji yalianza kuibuka Agosti 21 baada ya kutekwa watoto wanne.
Watoto wawili Ayoub Fred na Bakati Selemani wakazi wa eneo la FFU, kata
ya Murieti jirani na kata ya Olasiti walirejeshwa
0 Maoni:
Post a Comment