Neymar alifunga bao mechi yake ya
kwanza katika klabu yake mpya ya Paris St-Germain baada ya kununuliwa
kwa rekodi ya dunia ya £200m kutokaBarcelona.
Jordan Ikoko alifungua ukurasa wa mabao kwa kujifunga baada ya pasi ya Neymar kwa Edinson Cavani kuzimwa
Neymar kisha alimsaidia Cavani kufunga kwa pasi safi kabla ya nyota huyo wa uruguay naye kumpa pasi Neymar ambaye alifunga dakika za mwishomwisho akiwa hatua sita hivi kutoka kwenye lango.
Mchezaji huyo wa Brazil mwenye miaka 25 alichezeshwa upande wa kushoto lakini alihusika kati safu ya mashambulizi.
Alitamba sana uwanjani kwa kugeresha na kushambulia, ingawa mengi ya makombora yake yalizimwa kabla yake kufanikiwa kufunga dakika za mwisho.
0 Maoni:
Post a Comment