Staa wa Real Madrid Cristiano Ronaldo
anaweza kufungiwa kucheza mechi 4 mpaka 12 kwa kosa la kumsukuma vibaya mwamuzi
baada ya kupewa kadi nyekundu kwenye mchezo wa jana dhidi ya Barcelona.
Ronaldo alipata kadi 2 za njano ndani ya
dakika 3, kadi ya pili aliipata kwa kuonekana kujiangusha katika eneo la
penati.
Mchezaji huyo alichukizwa na maamuzi hayo
na kumsukuma mwamuzi kabla ya kutoka nje.
Mwamuzi Ricardo de Burgos Bengoetxea hakuonesha kuchukizwa na kitendo hicho lakini
alikijumuisha katika ripoti ya mechi na sasa Ronaldo anakabiliwa na hukumu
nyingine.
.
"Mara kadi nyekundu ilipooneshwa,
mchezaji (Ronaldo) alinisukuma mimi kwa ishara ya kutokukubaliana ".
Bengoetxea ameandika katika ripoti yake.
Sheria za shirikisho la soka la Hispania
zinasema " Vurugu ndogo kwenda kwa waamuzi kwa mfumo wa kunyakua,
kusukuma,au kutingisha inatakiwa kuadhibu kwa kifungo cha mechi 4 mpaka 12
".
0 Maoni:
Post a Comment