USIKU wa Jumatano, Saa 8 na Nusu kuamkia Alhamisi, Manchester United watatinga ndani ya Uwanja unaopakia Mtu 82,000 wa FedEx Field in Landover, Maryland, Washington DC, USA kuwavaa Vigogo wa Spain FC Barcelona.
Baada ya kuwatwanga Man City na Real Madrid, Man United wanasaka ushindi mwingine kwenye Mashindano ya International Champions Cup ambao utakuwa ushindi wa 5 katika Mechi zao za Ziara yao huko Marekani wakijitayarisha kwa Msimu mpya.
Katika Mechi zao 2 zilizopita za International Champions Cup, Man United waliitoa 2-0 Man City huko Houston Alhamisi iliyopita kwa Bao za Romelu Lukaku na Marcus Rashford na Jumapili walitoka Sare 1-1 na Real Madrid katika Dakika 90 na kuwabwaga kwa Penati 2-1 huku Bao la Man United likifungwa na Jesse Lingard.
Kabla, katika Mechi za Kirafiki, waliitwanga LA Galaxy 5-2 na kisha Real Salt Lake 2-1 kwenye Mechi ambayo Straika Mpya Romelu Lukaku alifungua Akaunti yake ya Magoli kwa kupiga Bao 1.
Ukiwaondoa Majeruhi, Ander Herrera na Juan Mata, Jose Mourinho anacho Kikosi kamili mbali ya Majeruhi wa muda mrefu Marcos Rojo, Luke Shaw na Ashley Young ambao wote wapo Kambini huko USA wakifanya Mazoezi kipekee.
Akiongelea matayarisho yao huko USA, Jose Mourinho ameeleza: “Hizi Siku 3 hapa DC si tatizo. Baada ya hapo tuna Mechi huko Norway na Ireland, tukisafiri Siku hiyo hiyo kwa masafa mafupi. Nimefurahia matayarisho yetu. Ikiwa Mata na Ander si Majeruhi wa muda mrefu basi ntasema kila kitu safi mno!”
Kwa Barcelona, Mechi hii na Man United itakuwa ni yao ya pili kuelekea Msimu mpya baada kuanza kwa kuichapa Juventus 2-1 Majuzi kwa Bao za Neymar.
Baada Mechi hii na Man United, Barca watawavaa Mahasimu wao Real Madrid Jumamosi huko Miami kwenye Mashindano haya ya International Champions Cup.
Wakati Man United wakikipga na Barca, Mahasimu wa Timu hizo mbili Real Madrid na Man City nao watapambana kuanzia Saa 12 Asubuhi ya Alhamisi huko Los Angeles Memorial Coliseum kwenye Mashindano haya haya ya International Champions Cup.
Timu hizo zote zilitoka kapa Mechi zao za kwanza kwa kufungwa na Manchester United.
Manchester United – Mechi zao kuelekea Msimu Mpya:
15 Julai v LA Galaxy, Stubhub Centre, Los Angeles [5-2]
17 Julai v Real Salt Lake, Rio Tinto Stadium, Sandy, Utah [2-1]
20 Julai v Manchester City, NRG Stadium, Houston, Texas (International Champions Cup) [2-0]
23 Julai v Real Madrid, Levi’s Stadium, Santa Clara, California (International Champions Cup) [1-1, Penati 2-1]
26 Julai v Barcelona, FedExField, Washington DC (International Champions Cup)
30 Julai v Valerenga, Ullevaal Stadium, Oslo
2 Agosti v Sampdoria, Aviva Stadium, Dublin
8 Agosti v Real Madrid, National Arena Filip II, FYR Macedonia (UEFA Super Cup)
0 Maoni:
Post a Comment