Kipa
Aishi Manula yupo njia panda kujiunga na timu yake mpya ya Simba
iliyoweka kambi nchini Afrika Kusini huku akipanga kuwapigia simu
viongozi wa Azam FC ili ajue taratibu za kuingia kambini.
Manula
ni kati ya wachezaji wapya waliosajiliwa na Simba kwa ajili ya msimu
mpya wa Ligi Kuu Bara uliopangwa kuanza kutimua vumbi Agosti 26, mwaka
huu licha ya mwenyewe kufanya siri.
Kipa huyo, anafanya siri kutokana na mkataba wake na Azam kutarajiwa kumalizika mapema mwezi Agosti, mwaka huu.
Manula
alisema kuwa yeye bado ni mchezaji halali wa Azam mwenye mkataba, hivyo
ni ngumu kwake kuihama timu hiyo kutokana na kanuni za usajili kumbana.
Alisema,
amepanga kuwasaliana na meneja wa timu hiyo, Philipo Alando kwa njia ya
simu na kikubwa kujua taratibu za kujiunga na kambi ya Azam iliyopo
Njombe ikiendelea na mechi za kirafiki.
"Niseme
tu ukweli mimi bado mchezaji halali wa Azam mwenye mkataba unaoelekea
ukingoni mwezi ujao, hivyo kila kitu kitajulikana baada ya mkataba
kumalizika.
"Hivyo,
nilichokipanga kukifanya hivi sasa ni kuwasiliana na meneja wa timu ili
nijue utaratibu wa kujiunga na kambi ya Azam iliyopo Njombe.
"Ninaheshimu mkataba wangu na nisingependa nitofautiane na timu yangu,"alisema Manula kipa namba moja wa Taifa Stars.
0 Maoni:
Post a Comment