Manchester United sasa wana 'zana bora' za kutwaa Ubingwa wa England Msimu huu mpya unaoanza Agosti lakini kwenye UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI bado wanahitajika kuwa 'bora zaidi' kwa mujibu wa Meneja wao machachari Jose Mourinho.
Msimu uliopita, ukiwa ni Msimu wa kwanza kwa Mourinho kushika
hatamu Old Trafford, Man United walitwaa Ngao ya Jamii, Kombe la Ligi,
EFL CUP, na UEFA EUROPA LIGI ambalo limewawezesha kuingizwa Makundi ya
UCL Msimu huu ujao licha kushika Nafasi ya 6 kwenye EPL, LIGI KUU
ENGLAND.
Akihojiwa na BBC Sport hapo Jana kama Man United wanalenga kutwaa
Ubingwa wa EPL Msimu huu mpya, Mourinho alijibu: "Sasa tupo tayari
zaidi!"
Kwa ajili ya Msimu mpya, Man United imewasajili Wachezaji Wapya Romelu Lukaku na Victor Lindelof.
Mourinho ameeleza: "Msimu utakuwa mgumu lakini nadhani sasa tupo
imara zaidi kupigania Ubingwa. Nadhani sasa tuna zana bora zaid. Lakini
tunapigana na Timu bora zaidi zilizowekeza bora zaidi. Lakini nakiamini
Kikosi changu, ari yetu, nia yetu, mshikamano wetu. Nawaamini Vijana
wangu na tutajaribu!"
Aliongeza: "Tulienda EUROPA LIGI.kama moja ya Timu kubwa, sasa
tunaenda CHAMPIONZ LIGI na hatupo kwenye Timu kubwa. Inabidi tufanye
vyema zaidi huko. Kitu muhimu ni kusaka Timu yenye furaha na kuelewana."
Pia alisema: "Nina furaha na Kikosi changu lakini napenda kuongeza
Wachezaji Wawili zaidi. Kiungo atanipa uwezo zaidi wa kutumia mifumo na
mbinu nyingi zaidi. Mwingine ni Fowadi anaeshambulia toka kwenye Wingi
ili nipate upana zaidi wa mashambulizi."
Mourinho amesisitiza hana wasiwasi na kupata hao wapya na yeye anasubiri 'habari njema' tu toka kwa Mtendaji Mkuu Ed Woodward.
0 Maoni:
Post a Comment