Nahodha wa Manchester United amekubali kujiunga na klabu yake ya zamani ya Everton FC baada ya wakala wake kukamilisha mazungumzo na klabu hiyo iliyomkuza.
Everton FC itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa SportsPesa Super Cup Julai 13 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Taarifa
zimeeleza kuwa Rooney amejiondoa katika safari ya kwenda Marekani
ambako Man United itafanya mazoezi kujiandaa na msimu mpya.
Chanzo
kutoka Old Trafford kimeliambia Gazeti la The Sun la Uingereza kwamba
usiku wa kuamkia jana, kila kitu kilikamilishwa kuhusiana na
makubaliano.
Akiwa
na Man United, Rooney ametupia mabao 253 kambani na alijiunga nayo kwa
kitita cha pauni milioni 26.5 miaka 13 iliyopita akitokea makao makuu ya
Everton, Goodison Park.
Kabla
kulikuwa na taarifa kwamba Rooney angekwenda Marekani au China kubeba
mamilioni ya fedha lakini suala la familia yake kuishi nchini humo
linaonyesha kutomfurahisha.
0 Maoni:
Post a Comment