LEO majira ya saa 12:00 jioni Tanzania watakua kwenye Mechi ya Nusu Fainali ya COSAFA CUP ambayo watacheza na Zambia huko Moruleng Stadium.
Tanzania wametinga Nusu Fainali baada ya Juzi kuwabwaga Wenyeji South Africa 1-0 kwa Bao la Dakika ya 18 la Elias Muguli wakati Zambia wakiitoa Botswana 2-1 kwenye Mechi za Robo Fainali.
Nusu Fainali nyingine ambayo itachezwa hii Leo baada ya Mechi ya Tanzania ni kati ya Lesotho na Zimbabwe.
Wakati Timu zilizoshinda Robo Fainali zikitinga Nusu Fainali, Timu zilizopteza Hatua hiyo zipo kinyang’anyiro cha kugombea Ngao na Jana South Africa waliipiga Botswana 2-0 na kutinga Fainali pamoja.
0 Maoni:
Post a Comment