STRAIKA wa Lyon ya France Alexandre Lacazette amemaliza upimwaji Afya huko Arsenal Jijini London na yupo mbioni sasa kukamilisha Dili ambayo haitakuwa chini ya Pauni Milioni 45 na kumfanya yeye awe Mchezaji wa Bei Ghali Klabuni hapo.
Awali, Arsenal waligomewa Ofa yao na Lyon kwa ajili ya Straika huyo Kimataifa wa France mwenye Umri wa Miaka 26 lakini Mazungumzo yakadumishwa.
Ada kamili ya Uhamisho, ukichanganya na Vipengele vingine vyote, inaweza kufika Pauni Milioni 52 na kuipita ile Arsenal walilipa Pauni Milioni 42.4 kumnunua Mesut Ozil kutoka Real Madrid Mwaka 2013.
Msimu uliopita, Lacazette ndie alikuwa Mfungaji Bora wa Ligi 1 huko France alikopiga Bao 28 na ameshapiga Jumla ya Bao 129 katika Mechi 275 tangu alipoanza kuichezea Timu ya Kwanza Msimu wa 2009/10.
Huko France, Msimu uliopita, ni Straika wa Paris St-Germain tu, Edinson Cavani, aliempiku kwa kufunga Bao nyingi kwa Mechi za Mashindano yote aliepachika Bao 35.
Lacazette, ambae ameichezea Timu ya Taifa ya France Mechi 11, alikuwa aende Atletico Madrid lakini Vigogo hao wa Spain walipata pigo baada ya Rufaa yao kupinga kufungiwa Kusajili Wachezaji Wapya walioiwasilisha CAS, Court of Arbitration for Sports, kutupwa chini na hivyo kubaki Kifungoni hadi Januari 2018.
Lacazette sasa anakuwa Mchezaji wa Pili kutua Arsenal katika Kipindi hiki baada ya Fulbeki wa Kushoto Sead Kolasinac, aliejiunga kutoka Schalke ya Germany.
0 Maoni:
Post a Comment