Siku
chache baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Prof. Lipumba
kuwavua uanachama Wabunge wanane wa Viti Maalum kisha Spika Ndugai
kuridhia uamuzi huo, jana July 27, 2017 Wabunge hao wamefungua kesi
katika Mahakama Kuu ya Tanzania.
Wabunge
hao wamefungua kesi hiyo iliyopewa namba 143/2017 kupitia Wakili wao
Peter Kibatala lakini hata hivyo bado haijapangiwa Jaji huku Wabunge hao
wakidai hawajapewa muda wa kujitetea.
Mbali
na kufungua kesi katika Mahakama Kuu Tanzania, pia wamekata rufaa ndani
ya Chama chao kupinga utekelezaji huo na kuiomba Mahakama isitishe
utekelezaji wa uamuzi wa kufukuzwa Uanachama wao.
0 Maoni:
Post a Comment