Tume
ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imesema kuwa haitegemei kufutiwa udahili
kwa wanafunzi kwa baadhi ya vyuo, kutawakosesha baadhi ya wanafunzi
watarajiwa nafasi au kozi walizodhamiria kwenda kuzisoma.
Akizungumza
kwenye Viwanja vya Maonesho, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana,
Ofisa Habari Mwandamizi, Edward Mkaku alisema TCU haitahusika na
wanafunzi ambao watakosa vyuo kwa sababu kwa sasa wameratibu udahili na
hivyo ni jukumu la mwanafunzi kutafuta chuo kulingana na ufaulu alionao.
“Hatutarajii
mwanafunzi kukosa chuo, na pia kufutiwa udahili kwa baadhi ya vyuo siyo
sababu ya wanafunzi kukosa nafasi kwenye vile vyuo vilivyopo,” alisema.
0 Maoni:
Post a Comment