Mawaziri
watano wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wametembelea
mpaka wa Tanzania na Uganda ili kutatua changamoto zinazoukabili mpaka
huo na kuuboresha.
Mawaziri
hao ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi,
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, Naibu Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Suleman Jaffo.
Pia
alikuwapo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Suzan Kolimba na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji,
Mhandisi Isack Kamwelwe.
Miongoni
mwa maeneo yaliyotembelewa na mawaziri hao jana Alhamisi, Julai 27 ni
eneo la mpaka ya Tanzania na Uganda kwa upande unapopita Mto Kagera na
eneo la kivuko cha mpaka wa Tanzania na Uganda kilichopo Mtukula mkoani
Kagera.
Katika
ziara hii mawaziri hao wameweza kujionea hali halisi ya maisha ya
wakazi wa mipakani na jinsi wanavyohusiana na wenzao wa nchi ya jirani
ya Uganda ambapo wamekuwa wakishirikiana na kuishi kwa amani katika
shughuli zao za kila siku.
Aidha,
ziara hii ni maandalizi ya mkutano wa ujirani mwema kati ya mawaziri wa
Serikali ya Uganda na mawaziri kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ambao unatarajiwa kufanyika Julai 29 , Bukoba mkoani
Kagera.
Jiwe la mpaka wa Tanzania na Uganda
0 Maoni:
Post a Comment