Watu
watano wameuwawa kwa kuchomwa moto katika kata ya Uchama Wilayani Nzega
Mkoani Tabora na watu wanaosaidikiwa kuwa ni Sungusungu huku wakidaiwa
wameuliwa kutokana na imani za kishirikina.
Kufuatia
Mauaji hayo Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Agreya Mwanri, amezitaka Kamati za
Ulinzi na usalama ngazi ya Mkoa na ile ya Wilaya ya Nzega kusitisha
shughuli zote zilizokuwa zikifanywa na sungusungu katika kijiji hicho.
Mwanri
amesema kuwa amechukua hatua hiyo baada ya sungusungu hao kutekeleza
mauaji hayo ya watu watano ambao wote ni wanawake wakituhumiwa kuwa ni
washirikina.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Wilbroad
Mutafungwa amesema kuwa katika kuendelea kuchunguza tukio hilo jeshi
hilo linawashikilia baadhi ya viongozi wa kijiji hicho ili kuweza
kubaini waliotekeleza tukio hilo.
0 Maoni:
Post a Comment