Katibu
Mkuu wa Chama cha CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema kwamba hatua ya
Spika kuwavua ubunge , udiwani na kuteua wengine wapya inalenga
kudhoofisha kambi ya wabunge wa CUF na Ukawa.
Amesema
Watanzania wanapaswa wajikumbushe kwamba hata kama hicho kinachoitwa
‘kuwafukuza uanachama’ wabunge halali wa CUF kingekuwa kiko sawa, hatua
kama hiyo hufuata taratibu zote za kisheria na kikanuni za Bunge
kujiridhisha kwanza.
“
Spika Job Ndugai anadhani Watanzania ni vichaa wamuamini kuwa
alishachukua hatua ya kujiridhisha kuwa wabunge wanane wa Chama cha
Wananchi (CUF) wamefukuzwa uanachama kulingana na taratibu za chama
hicho na hivyo wamekosa sifa za kuendelea na Ubunge. Ndani ya siku
moja?” amehoji Maalim.
Amesema
Spika amejiridhisha vipi ikiwa hata hakuwasiliana na Katibu Mkuu wa
Chama ambaye kwa mujibu wa Katiba ya CUF ndiye Mtendaji Mkuu wa shughuli
za chama na pia kwa nafasi hiyo ndiye katibu wa vikao vya Mkutano Mkuu
wa Taifa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama?
Amesema
yeye kama katibu, alimuandikia Spika Ndugai barua, Jumanne, Julai 25
akimueleza kwamba hilo lililoitwa Baraza Kuu la Uongozi la CUF
halikuundwa na wajumbe halali wa Baraza Kuu.
“Angekuwa
na nia ya kweli ya kutaka kujiridhisha si hapo ndipo pangekuwa pa
kuanzia kwa kuwepo kile wanasheria wanachokiita shaka inayoweza kuingia
akilini yaani ‘reasonable doubt’?’’ amehoji.
Amesema
Spika Ndugai aliyapuuza yote hayo kwa sababu ni kinyume na mkakati wa
Dola wa kuihujumu CUF na kuua demokrasia Tanzania. Hapo ndipo Spika Job
Ndugai alipolifikisha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
0 Maoni:
Post a Comment