Bado dirisha la usajili linaendelea kushika kasika kasi na
taarifa za chini chini zinadai kiungo wa Liverpool Phellipe Coutinho
amemuomba kocha wake Jurgen Klopp amruhusu kwenda Barcelona.
Inafahamika kwamba Barca wanaihitaji sahihi ya Coutinho na
wameshatuma ofa kwa Liverpool na wameshafanya mazungumzo na Coutinho
ambaye yuko tayari kujiunga nao wakati wowote.
Taarifa nyingine za usajili ni kwamba baada ya habari kuzagaa kwamba
Mbappe anakwenda Real Madrid sasa Pep Gurdiola maeingia katika mapambano
na anataka kutoa kitita kikubwa zaidi kwa Monaco ili kumnasa Mbappe.
Kocha wa Chelsea Antonio Conte amesema kwa sasa Harry Kane ndiye
striker anayemkubali sana nje ya Chelsea lakini hawezi kumnunua kwani
ana uhakika bei yake kwa sasa itakuwa iko juu sana.
Kiungo Jack Wilshaire hataki kuondoka nje ya jiji la London na anaona
kama Arsenal wataamua kumuuza ni bora wamuuze humo humo London huku
West Ham ikitajwa kama sehemu ambayo anaelekea Wilshaire.
Makamu wa raisi wa Monaco Vadim Vasylev amezikatisha tamaa klabu
zinazowataka Fabinho na Lemar kwa kusema kwamba wachezaji hao ni muhimu
na ana uhakika watabaki.
0 Maoni:
Post a Comment