Pambano la ngumi za kulipwa la Global TV limefanyika na kutia fora huku likirushwa LIVE na runinga hiyo ya mtandaoni.
Lilikuwa pambano kali na mabondia sita waliopigana kwa raundi zote 10 vizuri.
Mtanzania Nassibu Ramadhani alionyesha kiwango kwa kumchapa Yohane Banda wa Malawi.
Pambano hilo lilikuwa ni la kuvutia kutokana na ushindani kwa raundi zote kumi.
Katika pambano la pili la ngumi Iddi Pialali wa Tanzania alifanya kazi ya ziada kumshinda Regin Champion wa DR Congo.
Lilikuwa ni pambano kali kwa kuwa Champion alikuwa akipambana kuanzia mwanzo hadi mwisho wa pambano hilo.
Pambano
la tatu la la mwisho, liliisha kwa sare baada ya Francis Miyeyushi
‘Chichi Mawe’ kujirekebisha mwishoni dhidi ya Israel Kamwamba wa Malawi.
Kamwamba
ndiye alitawala raundi za mwanzo lakini Miyeyusho akaibuka na kupata
sare baada ya majaji wawili, mmoja kutoa ushindi kwa Kamwamba, mwingine
kwa Miyeyusho na mmoja akatoa sare.
0 Maoni:
Post a Comment