Skwadi
ya Simba ambacho kimepiga kambi nchini Afrika Kusini, ndani ya wiki hii
kitaanza kucheza mechi za kirafiki na timu mbalimbali zinazoshiriki
ligi kuu ya nchi hiyo.
Kikosi
hicho ambacho kiliondoka nchini Jumatatu ya wiki iliyopita, kwa wiki
nzima kimekuwa kikifanya mazoezi makali chini ya Kocha Mkuu Joseph Omog
pamoja na msaidizi wake, Jackson Mayanja.
Simba
ambayo itakuwa huko mpaka mwezi ujao, inatarajiwa kurejea nchini Agosti
6, mwaka huu kabla ya kufanyika kwa tamasha lao la Simba Day
litakalofanyika Agosti 8, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Akizungumza
kutoka Afrika Kusini, Mayanja alisema baada ya kufanya mazoezi ya nguvu
kwa wiki nzima, wanatarajia wiki hii kuanza kucheza mechi za kirafiki
bila ya kufafanua dhidi ya timu gani.
“Wiki
ijayo (wiki hii) ndiyo tunatarajia kuanza kucheza mechi za kirafiki,
mpaka sasa bado sijafahamu ni dhidi ya timu gani tutakazocheza nazo,
lakini mipango ipo hivyo.
“Kikubwa
ambacho naweza kusema, mazoezi yetu yanakwenda vizuri tukiwa na
wachezaji wachache ambao hawakuwa na majukumu na timu zao za taifa,
lakini muda wowote kuanzia sasa tunaweza kuwapokea wale waliokuwa Taifa
Stars pamoja na wachezaji wapya,” alisema Mayanja.
0 Maoni:
Post a Comment