Watafiti
nchini Marekani wanasema kuwa jaribio ambalo vijana wa Marekani
walitumia mpira wa mviringo kujilinda na virusi vya HIV limefanikiwa.
Utafiti zaidi sasa utafanyiwa vijana barani Afrika.
Wasichana
walitumia mviringo wa plastiki uliowekwa dawa za kujilinda na ukimwi ,
ambao hulibadilishwa kila mwezi baada ya kipindi cha miezi sita.
Ni
mojawapo ya mipango ya kutengeza kifaa ambacho wanawake watatumia
kujilinda dhidi ya maambukizi ya HIV ili wasiweze kuwategemea wanaume
kuvaa mipira ya kondomu.Wakiripoti ugunduzi huo mpya
kuhusu virusi vya HIV mjini Paris, watafiti walisema kuwa wanafurahi
kwamba wasichana hao walitumia mvirongo huo na kusema kuwa wameupenda.
Wanawake
na wasichana walio na kati ya umri wa miaka 15-24 wanadaiwa kuwa moja
kwa tano ya visa vyote vya maambukizi ya HIV duniani.
Takriban wanawake 1000 huambukizwa virusi kila siku katika Afrika ya jangwa la sahara.
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
0 Maoni:
Post a Comment