Klabu ya Monaco imeanza mazungumzo
ya kumuongezea kandarasi mshambuliaji wake Kylian Mbappe kulingana na
makamu wa rais wa klabu hiyo Vadim Vaslyev.
Mbappe ambaye ana kandarasi hadi mwezi juni 2019 amehusishwa na uhamisho wa Real Madrid.
Manchester
City pia imehusishwa ,lakini BBC Sport inaelewa kwamba hawako tayari
kulipa kitita cha Yuro milioni 180 za uhamisho wa mchezaji huo.
Vaslyev alisema kuwa klabu hiyo ya ligue One imepata maombi kuhusu mchezaji huyo.
Lakini ameongezea :Tunazungumza kuhusu kumuongezea kandarasi Kylian na kwamba tuna matumaini yakukubaliana.
Mbappe aliifungia Monaco mabao 26 katika mashindano yote .
Mapema mwezi Julai Monaco ilisema:Vilabu muhimu kutoka Ulaya viliwasiliana na mchezaji huyo bila ruhusa yao.
0 Maoni:
Post a Comment