Diego Maradona ameunga mkono
utumiaji wa kanda za video licha ya kukiri kwamba bao lake la ''Hand of
God'' dhidi ya Uingereza 1986 halikufaa kukubalika.
Maradona
alitumia mkono wake kufunga bao ambalo liliisaidia Argentina kuishinda
Uingereza 2-1 katika robo fainali ya kombe la dunia miaka 31 iliopita.
''Kwa kweli mimi hukumbuka bao hilo kila mara ninapounga mkono utumizi wa teknolojia'' ,Maradona aliambia Fifa.com.
''Nilifikiria kuhusu bao hilo na kwa kweli bao hilo halikufaa kuidhinihswa''.
Maradona anasema kuwa alifaidika kutokana na ukosefu wa teknolojia katika kombe la dunia na haikuwa mara moja bali mara mbili.
''Nitakwambia
kitu chengine -katika kombe la dunia la 1990 nilitumia mkono wangu
kuondoa mpira uliokuwa karibu kuingia katika goli letu dhidi ya taifa la
Usovieti.
''Tulikuwa na bahati kwa sababu refa hakuona.Hakukuwepo na teknolojia wakati huo lakini sasa ni mambo mengine''.
0 Maoni:
Post a Comment