MWAKA WA SHETANI!!! SANCHES APEPERUKA MANCHESTER UNITED

Manchester United inaelekea kumkosa kiungo wa Bayern Munich, Renato Sanches aliyekuwa akiwindwa na kocha Jose Mourinho.
 Kiungo huyo wa Kireno aliyeitosa Manchester United msimu uliopita na kuchagua kutua Bayern Munich, alihusishwa tena na safari ya Old Trafford kiangazi hiki baada ya Bayern kusema kuwa ipo tayari kumpiga bei mchezaji huyo. Hata hivyo Sanches sasa anaelekea kutua AC Milan baada ya gazeti la L'Equipe la Ufaransa kudai kuwa kinda huyo mwenye umri wa miaka 19, anakwenda San Siro kwa dau la pauni milioni 35. Gazeti hilo limedai Sanches atasaini mkataba wa miaka minne kuitumikia miamba hiyo ya Italia.
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment