TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Klabu
ya Simba kwa masikitiko makubwa inakanusha taarifa potofu zinazosambaa
mitandaoni na kwenye baadhi ya vyombo vya habari,kuwa imecheza mechi ya
kirafiki nchini Afrika kusini,na kupoteza mchezo huo.
Uzushi huo unasema Simba imefungwa mchezo huo kwa jumla ya goli 7-0, na timu ya daraja la kwanza ya nchini humo, Royal Eagles.
Kiukweli
Simba haina rekodi za hovyo kama hizo kokote inapocheza duniani,na
haijawahi kufungwa na klabu yoyote idadi ya magoli kama hayo,kama
zilivyo klabu nyingine nchini,hususan klabu ambayo mashabiki wake ndio
wanaozusha upuuzi huo.
Dunia
ya leo ni ya Teknolojia, na ingekuwa ni kweli,hakuna mtanzania ambae
asingeiona hii taarifa kutoka kwenye mitandao au vyombo vya habari vya
Afrika kusini.
Tunapenda
Umma wa watanzania utambue kwa siku zote tulizokuwa huko,program ya
benchi la ufundi, ilijikita ktk kuitengeneza miili ya wachezaji
kistamina.
Wiki
ijayo Timu yetu inatarajiwa kucheza mechi mbili na klabu za Orlando
Pirates na Bidverst za nchini humo, kabla ya kurejea tarehe tano mwezi
ujao teyari kwa mchezo wetu wa SIMBA DAY utakaopigwa tarehe nane mwezi
ujao.
Mwisho
Tunawaomba
wanachama na mashabiki wetu puuzeni uzushi wa mitandaoni, na taarifa
rasmi zitatolewa kwa mujibu wa taratibu rasmi za klabu.
IMETOLEWA NA..
HAJI S MANARA
MKUU WA HABARI WA SIMBA SC
SIMBA NGUVU MOJA
0 Maoni:
Post a Comment