Uongozi wa Klabu ya Singida United, umesema kuwa, wamepanga mechi zao za kwanza za nyumbani za Ligi Kuu Bara wachezee kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma kutokana na uwanja wao wa Namfua kutokuwa tayari.
Mechi
ambazo timu hiyo inaweza kucheza mkoani Dodoma ni dhidi ya Mbao
iliyopangwa kupigwa Septemba Mosi pamoja na ile dhidi ya Stand United
ambayo katika ratiba inaonyesha itachezwa Septemba 9. Mechi hizo zote
zilitakiwa kupigwa katika Uwanja wa Namfua ambao bado upo kwenye
matengenezo makubwa.
Katibu
wa klabu hiyo, Abdulrahman Sima, amesema: “Uwanja wetu wa Namfua bado
haujakamilika na sidhani kama ligi ikianza utakuwa tayari kutumika,
marekebisho yanayofanywa ni makubwa, zile nyasi zilizopandwa zinaendelea
kuota japo itakuwa haraka sana kuutumia.
“Kutokana
na hali hiyo, tumeliomba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ,kuturuhusu
kuutumia Uwanja wa Jamhuri uliopo Dodoma kwa mechi zetu za awali za
nyumbani mpaka pale uwanja wetu utakapokuwa tayari na TFF wamekubali
ombi letu.”
Timu
hiyo ambayo imepanda daraja hivi karibuni, Agosti 26, mwaka huu itaanza
mechi yake ya Ligi Kuu Bara ikiwa ugenini kucheza dhidi ya Mwadui FC
kwenye Uwanja wa Mwadui Complex.
A+
A-
Print
Email
KOCHA Mkuu wa Chelsea, Antonio Conte ameelekeza matumani yake kwa nyota
wake, Cesc Fabregas, baada ya kusema kuwa ana imani atakuwa tegemeo kwa
klabu katika kipindi cha msimu ujao.
Msimu uliopita licha ya kuwa na mchango mkubwa katika safu ya kiungo
nyota alikuwa akishindwa kupata nafasi ya kucheza mara kwa mra kwenye
kikosi cha kwanza ambacho kiliipa Chelsea ubingwa wa michuano ya Ligi
Kuu England.
Vile vile wakati Eden Hazard akiwa bado anauguza majeraha yake ya enka
mwaka huu kunaweza kukashuhuduwa mabadiliko makubwa katika safu ya
ushambuliaji.
"Ni mchezaji mzuri sana ambaye anaweza kucheza vizuri katika nafasi hii
ya kiungo, lakini vilevile ana uwezo wa kucheza namba 10," alisema
Conte.
"Ni mfano mkubwa kwa wenzake kutokana na anavyojituma na tabia yake ya
kila siku wakati wa mazoezi. Ni lazima ataendelea kuwa hivyo kutokana na
kwamba anatufanyia kazi nzuri,”aliongeza kocha huyo.
Alisema kwamba anavyoamini Cesc kwa sasa ameimarika zaidi tofauti na
alivyomkuta wakati alipowasili Chelsea na akasema kuwa ukimuangalia
tangu mwanzo na sasa unaweza kuona jinsi alivyoimarika zaidi.
Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2017/07/conte-asema-fabregas-atakuwa-tegemeo.html
Copyright © saluti5
Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2017/07/conte-asema-fabregas-atakuwa-tegemeo.html
Copyright © saluti5
LICHA ya kuwa na miaka mingi katika kibarua chake, straika Jermain
Defoe amesema kwamba amelenga kucheza tena katika fainali za Kombe la
Dinia akiwa na kikosi cha timu ya Taifa ya England.
Staa huyo kwa sasa amejiunga na timu ya Bournemouth akitokea
Sunderland, baada yap aka hao weusi kushuka daraja katika Ligi Kuu
England,lakini anasema kuwa mawazo yake yote kwa sasa ni kuwamo kwenye
kikosi hicho cha kocha Gareth Southgate kitakachcheza fainali hizo za
mwakani zitakazofanyika nchini Russia.
Wakati wa fainali hizo za mwakani zinafanyika, Defoe ambaye msimu
uliopita alifunga mabao 15 atakuwa na umri wa miaka 35 na hiyo
itakuwa ni mara yake ya pili kucheza fainali hizo ikiwa ni baada ya
kucheza nyingine zilizofanyika nchini Afrika Kusini miaka saba
iliyopita.
"Ni jambo la kawaida kwa kila mmoja kutupia jicho kwenye fainali za
Kombe la Dunia,"alisema Defoe.
"Kila mchezaji nchini England anapenda kupata nafasi kwenye kikosi
hicho, lakini inategemea na na jinsi unavyocheza kwenye klabu
yako,”aliongeza tena.
Alisema kwamba kutokana na hilo ataendelea kuelekeza nguvu zake katika
hilo na endapo atapata nafasi ya kucheza kwenye fainali ndotyo yake
itakuwa imekamilika.
Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2017/07/defoe-awaza-kukipiga-fainali-za-kombe.html

0 Maoni:
Post a Comment