Msemaji
wa Ikulu ya Marekani, White House, Shawn Spicer, amejiuzulu wadhifa
wake kwa madai ya kupinga mabadiliko ya Timu ya Mawasiliano ya Ikulu
hiyo.
Bw.
Spicer ameachia wadhifa huo, kwa sababu hakufurahishwa na uamuzi wa
kumteua, Anthony Scaramucci kuwa Mkrugenzi mpya wa Mawasiliano wa Ikulu,
Mabadiliko
hayo yanafanyika wakati White House ikikabiliwa na uchunguzi kuhusu
tuhuma za Urusi kuingilia uchaguzi mkuu wa Marekani wa mwaka jana.
Gazeti
la New York Times linaarifu kwamba, Bw. Spicer alipinga vikali uteuzi
wa Bw. Scaramucci kama Mkurugenzi wa Mawasiliano akidai ni kosa kubwa.
Bw. Scaramucci, ameteuliwa kushika wadhifa huo baada ya aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo Mike Dubke kujiuzulu Mei mwaka huu.
0 Maoni:
Post a Comment