Waliojenga mpakani Tanzania na Zambia wapewa miezi 3

Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa.
WANANCHI waliojenga ndani ya eneo la mpaka wa Tanzania na Zambia, wamepewa miezi mitatu kuwa wamebomoa nyumba zao.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipotembelea eneo la ujenzi wa Kituo cha Pamoja cha Forodha (OSBP) katika mpaka wa Tanzania na Zambia jana jioni. Kituo hicho kinajengwa na Serikali ya Tanzania na kitagharimu Sh bilioni 12.

Aliigiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuanza kuweka alama za X katika nyumba 252 zilizojengwa ndani ya mpaka huo ili wahusika wazibomoe. “Kuna watu wamejenga ndani ya mpaka wa Tanzania na Zambia na kuendesha biashara zao jambo ambalo ni kinyume cha sheria na linazikosesha Serikali mapato,” alisema.

Aliagiza ndani ya miezi mitatu, watu wote waliojenga kuanzia umbali wa mita 50 kutoka Tanzania na mita 50 kutoka Zambia wawe wamezibomoa nyumba zao kwa hiari.

“Hatuna msamaha kwa watu waliojenga katika eneo hili kwa sababu wamesababisha tupoteze kodi nyingi, hivyo baada ya kumalizika muda huo mamlaka husika zibomoe nyumba zote zitakazosalia.”

Awali, Waziri Mkuu alikutana na Mkuu wa Wilaya ya Nakonde nchini Zambia, Field Simwinga ambaye alisema wamekubaliana na utekelezaji wa agizo hilo kwa kuwa jambo hilo linaathiri shughuli za mipakani kwa pande zote mbili

Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment