Hivi karibuni kumeibuka kwa
mauaji ya wananchi katika vijiji mbalimbali mkoani Iringa kutokanana na Uvamizi
wa Tembo katika makazi ya wananchi
sambamba na kuharibu mazao ya wakulima hasa katika vijiji vya Kisanga na
Itunundu.
Akizungumza na dmgidang.blogspot.com Mkuu wa wilaya ya Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela amesema hapo mwanzo
ilizoeleka kua Tembo hao walikua wakiingia katika mashamba ya wananchi na
kuharibu mazao lakini hivi sasa Tembo hao wamegeukia wananchi na kuwaua.
Amesema mpaka sasa watu wanne
wameripotiwa kuuawa na Tembo katika vijiji tofauti ikiwemo kijiji cha Chamdindi
kitongoji cha Fifi mnamo tarehe 25 mwezi
mei 2017 aliuawa mzee wa kimaasai maarufu kwa jina la Katamboi mwenye umri wa
miaka 60 ambaye ni mfugaji ailikua akitembea kutoka kijiji cha Izazi kwenda
Chamdindi alikumbana na Tembo na
kujeruhiwa kasha kukanyagwa na Tembo huyo na kuuawa.
Sambamba na hilo kijana mwanafunzi
wa darasa la pili Tyson Mdesa mwenye umri wa miaka 9 aliyekua anasoma shule ya msingi Chamdindi alikumbana
na Tembo wakati anatoka shule na akauawa.
Aidha katika kijiji kingine
cha Kisanga tarehe 11 mwezi 6 aliuawa Daudi Kizuku mwenye umri wa miaka 50
ambaye kabila lake ni Mgogo mfugaji alijeruhiwa vibaya na Tembo na baadae
kufariki wakati akikimbizwa hospitalini, na katika tukio lingine Tarehe 19
mwezi wa 6 mwaka huu usiku wa kuamkia tarehe 20 bwana Geofrey Mbuzi katika eneo
la Mbuyuni mashambani ambaye alikua amejeruhi mtu katika ugomvi na wakati
akikimbia ndipo alikumbana na Tembo akajeruhiwa na akafa.
Kasesela amesema kwasasa
wanashirikiana na watu wa KDU pamoja na TANAPA kwaajili ya kuwarudisha tembo
hao kutoka katika mazingira ya wananchi .
Ameongeza kuwa matukio haya
ya uvamizi wa tembo yanatokana na eidha kupungua kwa matukio ya ujangili ambayo
yanawapa nafasi Tembo kuzurula mbali zaidi au jambo lingine ni kutokana na
kupungua kwa vyanzo vya maji katika maeneo wanayoishi Tembo na kuamua kwenda
kutafuta maji sehemu nyingine.
0 Maoni:
Post a Comment