Hivi karibuni Kata ya
Kitwiru iliyopo manispaa ya Iringa wananchi wa eneo hilo waliweza kumuona chatu
mkubwa akiwa anaotea jua karibu na daraja lilipo barabara ya kwenda Mbeya na kumuua.
Akizungumza na dmgidange.blogspot.com
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Richard Atufigwege Kasesela
amewatahadharisha wananchi wa eneo hilo juu ya kuonekana kwa Chatu huyo ambapo
amesema inawezekana kukawepo na mwingine katika maeneo hayo.
Kasesela amesema ametuma
watu kwaajili ya kuchunguza eneo hilo ambalo Chatu huyo mkubwa mwenye unene
saizi ya mguu wa binadamu mtu mzima kubaini kua kama kuna Chatu mwingine.
Aidha Kasesela amewaomba
wananchi hao kuchukua tahadhari ya eneo hilo na kua makini mpaka watafiti hao
watakapotoa taarifa juu ya eneo hilo.
0 Maoni:
Post a Comment