Kampuni ya Kuchimba Madini ACACIA Iliingia Kinyemela na Wala Haina Kibali Chochote

Taarifa ya pili ya  wachumi na wanasheria iliyofanya uchunguzi wa madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga wa madini iliyoundwa na Rais Joseph Magufuli, imebaini kuwa kampuni ya ACACIA Mining Plc haina kibali na inafanya kazi kinyume cha sheria.

Prof. Osoro amesema kwamba  Kamati yake imebaini kuwa Acacia haina uhalali wa kufanya shughuli zake hapa nchini  na imetenda makosa yakiwemo kujipatia mali kwa udanganyifu, uhujumu uchumi, jinai na kuitia hasara taifa.

Aidha Kamati ya Prof. Osoro imebaini kwamba  Makinikia yaliyouzwa nje ya nchi hayakuwa makinikia hasa, bali yalikuwa ni madini mbalimbali huku ikiongeza kwamba  katika mikataba ya uuzwaji wa makinikia hayo, serikali haikuwa sehemu ya mikataba hiyo.

Prof. Osoro ameongeza kwamba jumla ya mapato yote ambayo serikali imepoteza ni Tsh. trilion 68.6 sawa na bajeti ya miaka miwili ya nchi kodi ya mapato ambayo taifa imepoteza ni Tsh. tril 55.07, mrahaba tril 11, bandari tril 1.6. na kwamba jumla ya thamani ya madini kwenye makontena yote 44,277 tangu mwaka 1998 ni Tsh. tril 132.56.

Pamoja na hayo imebainika kuwa uongezwaji wa leseni kinyume cha sheria ambapo imedaiwa kuwa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini  William Ngeleja na Sospeter Muhongo ndio waliohusika na uongezaji wa muda kwenye uchimbaji wa madini.

Kamati hiyo imetoa mapendekezo mbalimbali ikiwepo kuchukua sheria juu ya kampuni ya ACACIA iliyopo nchini kinyume cha sheria kupitia msajili wa makampuni ikiwa ni pamoja na Mawaziri wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine juu ya mikataba ya uchimbaji madini huku ikiitaka Serikali iwe inafanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye makampuni ya madini
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment