Mbunge
wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy amependekeza kuwapo na sheria ya
kuwapima wabunge matumizi ya dawa za kulevya ili kuepukana na ukorofi
unaojitokeza bungeni mara kwa mara.
Keissy
alisema hayo jana bungeni mjini Dodoma na kusisitiza kuwa yeye atakuwa
mstari wa mble kwenye upimaji na endapo itatokea mbunge yoyote yule
atakayebisha kupimwa kipimo hicho basi apimwe kwa nguvu na afukuzwe
ubunge.
"Tutengeneze
sheria sisi sote hapa tupimwe, inawezekana kuna watu wanatumia madawa
ya kulevya humu, tena mimi nitakuwa wa kwanza, tupimwe kuondoa tatizo
kwenye bunge letu hili la ukorofi na atakayekataa apimwe kwa nguvu na
afukuzwe ubunge haiwezekani kurudia makosa mtu mmoja kila siku anasemwa
anarudia yale yale" alisema Keissy na kuongeza;
"Adhabu
ndogo hii lazima ziwe kali wasipate chochote, wasionekane bungeni muda
wa miezi sita au saba ndiyo watashika nidhamu katika bunge hili.
Haiwezekani tunaonekana kama tupo Manzese, wabunge wa mjini wamezoea
kwenye vijiwe sisi wabunge wa bara hatutaki mchezo mchezo namna hii ya
kutukana. Spika kwanza anawazidi umri pamoja na cheo"
0 Maoni:
Post a Comment