Kanisa moja katika mji mkuu wa
Ghana, Accra, limeandaa ibada ya kutoa shukrani kutokana na ufanisi wa
hivi majuzi wa Chelsea katika Ligi ya Premia.
Alisimama juu ya keki ya Chelsea kwenye jukwaa ambalo lilikuwa limejengwa kufanana na uwanja wa soka.
Alisema: "Chelsea, kwa kudura zake Mungu, walimaliza wa kwanza."
Alisema kwamba alitaka kutumia nguvu za soka kuzungumzia kuhusu Mungu.
Azigiza pia aliongoza waumini kuimba aya ya wimbo wa klabu ya Chelsea, Blue is the Colour.
Pasta huyo, ambaye wakati mmoja alikuwa DJ wa redioni, alikuwa pia anamtania mkuu wake katika kanisa hilo la Living Streams International Church, Pasta Ebenezer Markwei, ambaye ni shabiki wa Arsenal, na ambaye alikuwa amemkaribisha kwa ibada hiyo
Alisema kuna mambo mema sana katika kfuurahia ufanisi wa watu wengine.
0 Maoni:
Post a Comment