MWAKA MMOJA JELA KWA TUHUMA ZA WIZI


JESHI la polisi mkoani Songwe linawashikilia watu nane  jinsia ya kiume wote wakiwa  wakazi wa kijiji cha Malezi wilaya ya Songwe mkoani hapa kwa tuhuma za uvuvi haramu ambapo wamekutwa na nyavu aina ya kokolo pamoja na vyandarua katika ziwa Rukwa. 

Tukio hilo   limegundulika  kufuatia msako mkali uliofanywa na jeshi la polisi huko ziwa rukwa ambapo watuhumiwa hao walikamatwa na nyavu kumi pamoja na vyandarua ambavyo wanatumia kuvulia samaki.

Akizungumza  na  kituo  hiki  ofisini kwake,kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Songwe Ambwene Mwanyasi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa watuhumiwa wote tayari wamekamatwa na juhudi za kuwafikisha mahakamani zinaendelea.

Aidha juhudi zakuwatatafuta watuhumiwa wengine ambao wametelekeza nyavu zao na mitumbwi zinaendelea,mbao walikimbilia kusikojulikana baada ya kuona kuna doria ya kushitukiza katika ziwa hilo.

Mwanyasi ametoa wito na kuwataka wavuvi wengine haramu waache mara moja kwani jeshi la poli litaendelea na mskao dhidi ya wote wanaojihusisha na uvuvi haramu kwenye mwambao wa Kamsamba ziwa Rukwa.

Katika hatua nyingine mahakama ya mwanzo vwawa mjini imemuhukumu kifungo cha nje mwaka mmoja liliani amosi 31 mkazi wa ilembo vwawa wilaya ya mbozi mkoani songwe kwa kosa la wizi wa mahindi kinyume na kifungu cha sheria 265 kanuni ya adhabu sura ya 16.

Akisomewa hukumu hiyo mahakamani hapo na hakimu wamahakama hiyo ediga mwaiswaga amesema kuwa ametoa adhabu hiyo kwa mshitakiwa ili iwe fundishio kwa watu wengine wenye nia ya kufanya tukio kama hilo.

Awali akisomewa shitaka hilo mahakamani hapo na mwendesha mashtaka wa jeshi la polisi nurdin mmanga mbele ya hakimu wa mahakama hiyo ediga mwaiswaga amesema kuwa mshitakiwa alikamatwa na mahindi debe mbili mali ya bahati joeli huku akijua kufanya hivyo ni kosa na kinyume cha sheria.

Mshitakiwa alipopewa nafasi ya kujitetea ameiomba mahakama impunguzie adhabu kwani yeye ni yatima na ana watoto watano  wanao  mtegemea
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment