Katika
kuhakikisha Jiji la Dar es salaam linakuwa katika hali ya usalama kwa
wananchi na mali zao, Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es
salaam, Simon Sirro amewatahadharisha wafanyabiashara wa CD ambazo zina
viashiria vya ugaidi kuacha mara moja biashara hiyo vinginevyo hatua
kali zitachuliwa dhidi yao.
Amesema
hayo Jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari, amesema kama wasipotii amri hiyo ya kuacha kuuza CD hizo zenye
viashiria vya ugaidi ndani yake basi Jeshi la Polisi litaanzisha msako
mkali dhidi yao na kuwachukulia hatua kali za kisheria.
“Hizi
CD zina viashiria ambavyo vinahamasisha watu kufanya uhalifu kama
ujambazi na masuala ya ugaidi, natoa angalizo kwa wafanyabiashara hao
kuziteketeza, hii ni kwa ajili tu ya kuliweka Jiji letu katika hali ya
usalama zaidi,”amesema Sirro.
Aidha,
katika hatua nyingine, Sirro amewataka wafanyabishara wote wa CD
wanaotandaza kando kando ya barabara kuacha mara moja kwani siyo sehemu
sahihi na salama ya kufanyia biashara hiyo.
Hata
hivyo, amesema kuwa hatua mbali mbali zinaendelea kuchukuliwa za
kuhakikisha Jiji linakuwa salama na shwari, pia ametoa wito kwa wazazi,
walezi, viongozi wa dini na wananchi kwa ujumla kufuatilia nyendo za
watoto wao ili wajue wanajishughulisha na nini.
0 Maoni:
Post a Comment